Exodus 23:1-6

Sheria Za Haki Na Rehema

1 a“Usieneze habari za uongo. Usimsaidie mtu mwovu kwa kuwa shahidi mwenye nia ya kudhuru wengine.

2 b“Usifuate umati wa watu katika kutenda mabaya. Unapotoa ushahidi kwenye mashtaka, usipotoshe haki ukijumuika na umati wa watu, 3 cnawe usimpendelee mtu maskini katika mashtaka yake.

4“Kama ukikutana na maksai au punda wa adui yako anapotea, hakikisha umemrudisha kwake. 5 dUkiona punda wa mtu anayekuchukia ameanguka na mzigo wake, usimwache hapo alipoangukia; hakikisha kuwa umemsaidia.

6 e“Usiwanyime haki watu wako walio maskini katika mashtaka yao.
Copyright information for SwhKC